loader
Picha

Chuo Kikuu Mzumbe chaboresha miundombinu kuongeza udahili

KATIKA kuhakikisha serikali inaboresha wigo wa udahili kwa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu, imeboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo Morogoro kwa kujenga mabweni manne katika eneo la Maekani Kampasi Kuu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Reinfrida Ngatunga alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo katika maonyesho ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Alitaja miundombinu hiyo kuwa ni mabweni, kumbi za mihadhara, madarasa, ofisi na nyumba za wafanyakazi kwa ajili ya kuimarisha mazingira hayo ya kujifunzia na kufundishia.

“Hii imetokana na utekelezaji wa miradi mitatu mikubwa ya ujenzi pamoja na miradi mbalimbali ya ukarabati iliyofanyika katika Kampasi zote tatu za Chuo Kikuu Mzumbe,” alisema. Alisema katika Kampasi Kuu, chuo hicho kinajenga majengo manne ya mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,024 kwa ufadhili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo imetoa sh. bilioni 6.5 mradi unaotarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi