loader
Picha

Chuo Kikuu OUT chaja na habari njema kwa waajiriwa

CHUO Kikuu Huria (OUT) kimesema kina wigo mpana wa fursa kwa wananchi wanaotaka kujiendeleza na elimu ya juu kwa kuwa kinatoa nafasi kwa wale wasiokuwa na ruhusa kazini kupata elimu ya juu kwa kuwa sio lazima mwanafunzi kukaa darasani.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko chuoni hapo, Dk, Mohamed Maguo alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo kwenye maonyesho ya elimu ya juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Alisema kwa takwimu zinaonyesha kuwa wananchi wanaonufaika na elimu ya juu ni ndogo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa ruhusa kazini.

Akimnukuu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema takwimu za kimataifa za ushiriki wa elimu ya juu zinaonesha kufikia mwaka 2017 ni asilimia moja hadi tatu tu ya watu kila kundi la Watanzania 100 wenye umri chini ya miaka 25 ndio wanaopata elimu ya chuo kikuu.

Pia kama Chuo Kikuu Huria nchini kimejipanga kutoa bidhaa bora ya wasomi ambao wataweza kuendeleza viwanda kwa kutoa kozi zinazomwezesha mwanafunzi kujiajiri baada ya kumaliza elimu yake pasipo kusubiri kuajiriwa katika kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya Viwanda ifikapo 2025.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi