loader
Picha

Stars ni bandika bandua Afcon

MABADILIKO ya ratiba ya mechi za kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika, Afcon yaliyofanywa na Shirikisho la soka Afrika, CAF yataifanya timu ya taifa, Taifa Stars kuwa na nafasi finyu ya kupumzika kwani italazimika kucheza mfululizo.

CAF imekuwa na mkutano wake wa kamati ya utendaji na kufanya mabadiliko ya mechi za kufuzu fainali za Afcon mwaka 2021zilizopangwa kufanyika Cameroon. Taarifa ya Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo kwa vyombo vya habari jana, mechi za kwanza za kuwania kufuzu sasa zitachezwa mapema, Oktoba 7 mpaka 15 mwaka huu.

Stars itawania kufuzu fainali za Afcon kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu huu kushiriki fainali za Misri na kuishia hatua ya makundi. Tanzania imefuzu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Kwa mujibu wa Ndimbo, kamati ya utendaji ya Caf iliyokutana Cairo Misri juzi, ilipanga raundi nyingine ya mechi hizo ichezwe Novemba 11 mpaka 19 mwaka huu. “Raundi nyingine itachezwa Agosti 31, 2020 mpaka Septemba 8, kabla ya raundi nyingine kuchezwa kati ya Oktoba 3-15 na raundi ya mwisho itachezwa Novemba 9-17 2020’’.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi