loader
Picha

Azam FC yasaka rekodi Kagame

MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame, Azam FC leo wanashuka dimbani mjini Kigali, Rwanda kusaka rekodi nyingine ya kucheza fainali dhidi ya As Maniema ya DR Congo.

Azam FC ilifika hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa TP Mazembe kwa mabao 2-1 huku Maniema ikiwatoa wenyeji APR kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kucheza dakika 90 bila kufungana.

Akizungumzia mchezo huo muhimu, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema tayari wamewasoma wapinzani wao na wameona nguvu yao sehemu ilipo na kujipanga dhidi yao.

“Tumeona nguvu yao ilipo na leo asubuhi (jana) tumelifanyia kazi kwa kuwapa mbinu wachezaji wetu namna ya kuwakabili na kupata matokeo,” alisema.

Alisema ili kutimiza ndoto yao ya kutetea ubingwa kikubwa ni Watanzania waendelee kuwaunga mkono na wao wamejipanga kuwakilisha vizuri.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi