loader
Picha

Mambo muhimu kuhusu fainali ya Algeria, Senegal

MAMBO matano ya kufahamu kuhusu timu mbili zinazopambana leo katika fainali ya Michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, Algeria na Senegal itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.

ALGERIA Nahodha na winga Riyad Mahrez kutoka Manchester City ndiye mchezaji pekee wa Algeria anayewakilisha Ligi Kuu ya England. Mchezaji mwingine wa Algeria anayecheza soka England, ni kiungo Adlene Guedioura, lakini yeye yuko katika klabu ya Ligi Daraja la pili ya Nottingham Forest.

Timu hiyo ina wachezaji saba wanaosakata soka nchini Ufaransa, wakiwemo mabeki Ramy Bensebaini na Mehdi Zeffane kutoka klabu ya Rennes, na watatu wengine kutoka Italia na Saudi Arabia.

Guedioura ndiye mchezaji mkongwe zaidi katika kikosi hicho cha timu ya taifa ya Algeria akiwa na umri wa miaka 33 na Hicham Boudaoui, ndiye mchezaji pekee katika kikosi hicho anayecheza soka nchini mwao na ana umri wa miaka 19 tu. FAINALI TATU Algeria imecheza fainali mbili zilizopita za Mataifa ya Afrika na zote ikikutana dhidi ya Nigeria. na walifungwa 3-0 jijini Lagos mwaka 1980 na kushinda bao 1-0 huko Algiers miaka 10 baadae.

Timu nyingi za mataifa ya Afrika zinachagua majina ya wanyama kuwa majina yao ya utani na Algeria ni miongoni mwao baada ya kuchagua jina la Mbweha na kujulikana na Mbweha wa Jangwani.

SENEGAL Nahodha na beki wake Cheikhou Kouyate (Crystal Palace), kiungo Idrissa Gueye (Everton) na mshambuliaji nyota Sadio Mane (Liverpool) wanacheza katika Ligi Kuu ya England. Kikosi cha Senegal kina wachezaji wanane wanaocheza soka nchini Ufaransa, akiwemo kipa Abdoulaye Diallo na washambuliaji Mbaye Niang na Ismaila Sarr kutoka Rennes.

Mabeki Saliou Ciss kutoka klabu ya Daraja la Pili Ufaransa ya Valenciennes ndiye mchezaji mkongwe zaidi katika kikosi hicho akiwa na umri wa miaka 30 na mshambuliaji Krepin Diatta kutoka klabu ya Brugge ndiye chipukizi zaidi akiwa na miaka 20.

Hii ni fainali ya pili ya Senegal baada ya ile ya kwanza, ambapo walifungwa kwa penalti na Cameroon mwaka 2002 baada ya kutoka suluhu licha ya kuongezewa muda huko Bamako. Timu yao ya taifa inajulikana kwa jina la utani kama Simba wa Teranga. Teranga ina maana ya ukarimu lugha maarufu sana kwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi