loader
Picha

Kocha Ghana anusurika kichapo

KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah amenusurika kuumia baada ya kuvamiwa na kijana mwenye hasira jijini hapa wakati akiendesha gari katika foleni.

Anashukuru alikuwa amefunga vioo vya madirisha ya gari lake, Kwesi Appiah aliambulia matusi na kashfa kutoka kwa kijana huyo, ambaye hajatambulika. Shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa tukio hilo, ambalo lilitokea katika daraja jipya lililofunguliwa katika barabara ya chini, ambayo linaunganisha Spintex kwenda Legon Mashariki lilikuwa la aibu kubwa.

Kocha huyo alikuwa katika gari lake aina ya Toyota SUV la mwaka 2015 wakati akielekea Legon Mashariki wakati kijana huyo alipombaini. “Wewe ni kocha? Mpumbavu sana wewe. Kwa Ghana nzima wewe huna maana kabisa.

Hatukutaki wewe kuwa kocha wa timu ya taifa,” alisema kijana huyo aliyekuwa na hasira kali. Akizungumza katika lugha yake ya Fante, aliendelea kumtukana Kwesi Appiah wakati magari yakienda taratibu katika foleni, akisema, “Nani kakwambia wewe ni kocha? Goigoi, huna akili.

Hujui lolote kuhusu soka na kufundisha soka.” Madereva wengine katika eneo hilo walijaribu kumpoza kijana huyo na Appiah alipata upenyo katika foleni na kuondoka taratibu na gari lake.

Alijidai kama amepokea simu wakati matusi na maneno ya kashfa yakizidi kutolewa na kijana huyo. Mtindo wa Appiah katika mechi za Ghana za Afcon 2019 zimekuwa gumzo tangu Black Stars itolewe kutoka katika michuano hiyo ya Afcon nchini Misri katika raundi ya 16 bora.

Baada ya kuwasili nyumbani, usalama wa Appiah ndio ulikuwa gumzo siku chache zilizopita, huku mtu mwingine mwenye hasira nusura aingie nyumbani kwa kocha huyo akiwa na lengo la kumvamia.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: ACCRA, Ghana

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi