loader
Picha

Costech pekee inatoa vibali vya utafiti nchini

TUME ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ndiyo pekee inayotoa vibali kwa watafiti wote waTanzania na wageni kwa ajili ya kufanya utafiti.

Msajili wa Vibali vya Tafiti kutoka Costech, Sylvia Mkala alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo katika maonyesho ya Elimu ya Juu ya 14 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa vyuo vikuu, wanafunzi ama watafiti endapo watataka kupata vibali hivyo sehemu ya pekee ni katika tume hiyo.

Katika hatua nyingine, Kaimu Ofisa Habari kutoka tume hiyo, Deusdedith Leonard alisema Costech ina majukumu ya kukusanya, kuhifadhi na kusambaza matokeo ya utafiti na ubunifu hapa nchini.

Alisema tume hiyo ipo kwenye maonyesho hayo ili kujulisha umma na kuwaonyesha kazi wanazozifanya kama Idara ya Menejimenti ya Maarifa kwenye tume hiyo ambayo inatoa matokeo ya tafiti mbalimbali zenye majibu ya changamoto mbalimbali zinazofanyika hapa nchini.

“Tunaandaa mikutano mbalimbali ya kimataifa, maonyesho na kuandaa makongamano na waandishi wa habari kuwaambia vyanzo vya kupata taarifa za kitafiti na namna gani wanaweza kuandika habari hizo,” alisema.

Alitoa mfano kuwa wameshakutana na waandishi wa habari wa Zanzibara pamoja na Mtwara, sasa wanatarajia kwenda Dodoma na Tanga.

“Kwa kutambua umuhimu wa waandishi wa habari tunaita watafiti wenye matokeo chanya na kuwaunganisha nao kwa ajili ya kuandaa makala,” alisema.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi