loader
Picha

Lukuvi atamani wanyonge wamiliki ardhi

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekemea tabia ya baadhi ya halmashauri kuuza viwanja kwa bei jambo ambalo amesema itakuwa vigumu masikini kumilika ardhi iliyopangwa.

Lukuvi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wataalamu wa ardhi nchini wapatao 800 ambao wamekutana jijini hapa kwa kwa siku tatu. Alisema tabia ya halmashauri kuuza viwanja kwa bei kubwa kwa lengo la kupata mapato ya ndani mengi, ni kero kwa wananchi na kusisitiza hali hiyo itafanya wanaoendelea kumiliki ardhi kuwa ni matajiri na masikini kushindwa kumudu Lukuvi alihimiza uwepo wa bei elekezi ya upimaji wa viwanja na mashamba.

“Hivi sasa baadhi ya halmashauri zina uza viwanja kwa bei kubwa sana isiyolingana kabisa na gharama walizoingia kwa tamaa ya kupata mapato mengi ya ndani. Kuna wimbi sasa kila halmashauri inajivuna tumepata fedha nyingi, wamelanga kwenye ardhi, hii hapana, hakuna ulanguzi wa ardhi hapa…ninyi halmashauri mna ardhi, lakini hatukuwaambia muwe nyarubanja mlangue bei mnayoitaka, sasa tutaingilia kati, tunataka watalaamu wa ardhi msimamie na kuelekeza bei,” alisema.

Waziri Lukuvi aliongeza kuwa wanafanya tathimini na gharama zote kwa Sh 100, halafu wanataka wapate Sh bilioni moja, matokeo yake wanaongeza kero kwa wananchi na wasiokuwa na fedha wataendelea kuwa na makazi holela tu.

“Wataona bora kuendelea kujenga mahali ambapo hapajapangwaa maana ni rahisi zaidi kuliko viwanja vyako vilivyopangwa. Kwa hiyo suala hili la uuzaji wa viwanja na upangaji ni zuri lakini lazima liwekewe utaratibu ili viwanja vyenyewe viuzwe kwa bei inayohimilika, isiwe kila mtu tu anaamua, umasikini wote na posho zote za madiwani na wilaya zitokane na uuzaji wa viwanja haiwezekani. Yaani umasikini wote wa wilaya na madeni yenu myabambike kwenye ardhi, hapo mnafanya ardhi ionekane ni ya watu matajiri, masikini hawatamudu kununua viwanja vilivyopangwa,” alisema.

Waziri Lukuvi alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa ofisi za kanda za mikoa ambazo zinaanzishwa kushirikiana na halmashauri katika kukokotoa gharama za upimaji wa ardhi.

“Kwa hiyo wale watendaji wa ofisi yangu ya mkoani, watashirikiana na halmashauri kukokotoa gharama na kushauriana juu ya bei ya kuuzia kwa mradi na upimaji wa mashamba lazima uwe na bei elekezi. Wananchi wanataka kupima mashamba yao lakini wanaibiwa, maana anaweza kuja mpimaji mmoja anasema kupima eka moja ni Sh 300, nataka kila mkoa uweke vigezo vya gharama ya upimaji wa mashamba na gharama za upimaji wa viwanja, mkikaa sekretarieti ya mkoa mnaweza kuweka vigezo ili wananchi waweze kumiliki ardhi iliyopangwa na salama na kupewa nyaraka kwa gharama nafuu,” alisema.

 JESHI la Magereza nchini limetahadharisha wananchi kuhusu kuwepo kwa watu ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi