loader
Picha

Maonesho vyuo vikuu yakuna wahitimu kidato cha sita

WAHITIMU wa kidato cha sita wanaojindaa kujiunga na vyuo mbalimbali nchini wamevutiwa na kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU), hatua iliyotokana na maelekezo mazuri ya miradi iliyofanywa na wanafunzi wanaosoma chuo hicho waliopo katika maonesho ya vyuo vikuu yanayomalizika leo Dar es Salaam.

Hayo yalibainishwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi jana, Hadija Maulid alipokuwa akizungumzia tathmini ya maonesho hayo ya 14 ambapo pamoja na mambo mengine aliwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na chuo hicho ili waweze kutimiza malengo yao ya kufanya kazi katika sekta ya ardhi na ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Alisema tangu kuanza kwa maonesho hayo, wanafunzi wengi wanaotembelea banda lao wamekuwa wakipewa maelekezo mbalimbali juu ya namna na sifa zinazompasa mwanafunzi kujiunga na chuo hicho huku kivuti kikubwa kwao kikiwa ni uwepo wa wanafunzi wanaosoma chuo hicho wanaowaonesha miradi mbalimbali waliyoifanya kutokana na masomo wanayoyasoma chuoni hapo.

“Tunashukuru uwepo wa maonesho haya kwa kiasi kikubwa yamekisaidia chuo chetu kupata wanafunzi wengi wanaotaka kujiunga na chuo, lakini zaidi wengi wao wamekuwa wakivutiwa na uwepo wa baadhi ya wanafunzi wetu waliopo hapa kuonyesha miradi mbalimbali walioifanya, jambo linalowafanya kuwa na imani na kutamani kuwa sehemu ya wabunifu wa miradi hiyo” alisema Hadija.

Alisema katika maonesho hayo Chuo Kikuu cha Ardhi pia kimekuwa kikiwapa elimu wanafunzi wanaofika katika banda hilo ikiwemo ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na majanga mbalimbali yanayoihusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini sambamba na uhifadhi wa Ardhi na Sayansi ya Udongo kwa ujumla.

Maulid alisema pamoja na hayo pia wamekuwa wakiwahamisha wanafunzi hao kujiunga na chuo hicho ili kuongeza wataalamu katika idara za upimaji wa Ardhi, Uthaminishaji wa majengo, mazingira, mipango miji pamoja na ubunifu wa majengo huku kigezo kikubwa kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na ARU kikiwa ni ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi