loader
Picha

Mwanafunzi Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere abuni mfumo wa kuzuia gesi isivuje

Mwanafunzi Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere abuni mfumo wa kuzuia gesi isivuje Na Lucy Ngowi MHITIMU kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Ramadhani Abushiri amebuni teknolojia ya mfumo wa kuzuia gesi isivuje ambao lengo lake ni kuzuia ajali ya gesi pindi ikiwa inavuja.

Abushiri ambaye alimaliza hivi karibuni chuoni hapo, alisema amesomea stashahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo imemwezesha kubuni mfumo huo.

Alieleza mfumo huo jinsi unavyofanya kazi kuwa unawekwa katika nyumba, kisha ikitokea gesi inavuja mfumo huo utafunga mfumo wa gesi ili kuzuia gesi isiendelee kuvuja.

Alisema kwa ile gesi ambayo ilikuwa tayari imeshavuja haitaendelea kuwepo ndani kwa kuwa mfumo utaitoa nje kwa feni maalum ambayo itatumika kuvuta gesi iliyovuja ndani.

“Baada ya hapo mfumo utakutumia meseji kama mwenye nyumba kukutaarifu kama kuna hatari ya gesi kuvuja sambamba na hapo pia kengele itapiga kutaarifu watu waliokuwemo ndani,” alisema.

Alisema mfumo huo kwa sasa upo kwenye hatua ya elimu, endapo ukianza kutumika anawataka wananchi wachangamkie fursa hiyo kwa kuwa utaokoa maisha ya watu na mali zao.

Naye Mkuu wa Idara ya Masomo ya Elimu ya Juu chuoni hapo, Dk. Philip Daninga alisema chuo hicho kina mfumo wa kufundisha wanafunzi unaolenga vitendo ambao umesaidia kuwaelimisha vijana kuwa baada ya kuhitimu wasisubiri kuajiriwa.

“Upande wa Tehama tumesisitiza kufundisha kwa vitendo zaidi kwa sababu kuna tatizo la ajira,”alisema.

Alisema ulimwengu wa sasa unategemea Tehama, hivyo chuo kimejikita kuhakikisha kozi zinazofundishwa zinamsaidia mwanafunzi akihitimu awe mbunifu anayeweza kuangalia mazingira yanayomzunguka na kubuni kitu.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi