loader
Picha

Takukuru Moro yaokoa mil 464/- za Halmashauri

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Morogoro imeokoa Sh milioni 464 za serikali ambazo zilikuwa hazijapelekwa benki katika Halmashauri sita za wilaya za mkoa wa Morogoro zilizotokana na ukusanyaji wa mapato kwa njia ya mashine za PoS (Point of sale machine).

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Morogoro, Janeth Machulya alisema hayo jana katika taarifa yake kuhusu utekelezaji kazi za uchunguzi na uzuiaji wa mianya ya Rushwa kwa miezi mitatu, Aprili hadi Juni , 2019 Aliwaambia waandishi wa habari kuwa Takukuru mkoa pia inafuatilia miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Morogoro ambapo Serikali imetenga Sh bilioni 1.5 za ujenzi na mradi wa ukarabati wa majengo ya Shule ya Sekondari Morogoro unaogharimu zaidi ya Sh bilioni moja.

Alisema katika kuzuia rushwa, walifuatilia ukusanyaji mapato kwa mashine za PoS halmashauri za mkoa wa Morogoro na Takukuru imeokoa Sh 464,020,079 . 48 ambazo zilikuwa hazijapelekwa benki. Machulya alizitaja halmashauri za mkoa huo ambazo hazikuwasilisha fedha benki kuwa ni Manispaa ya Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kilombero, Kilosa, Mvomero pamoja na Gairo .

“Tulibaini wapo mawakala walioingia mikataba na halmashauri hawakuwasilisha fedha benki kwa mujibu wa sheria na watendaji wa halmashauri kushirikiana na mawakala kujipatia fedha,” alisema. Aliwaonya mawakala wa kukusanya mapato kwa mashine kuzifikisha fedha benki na watendaji wa serikali watakaobainika wanashirikiana kuchota fedha za umma, wachukuliwe hatua za kisheria.

Kuhusu ufuatiliaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Morogoro alisema Takukuru imebaini manunuzi yasiyozingatia taratibu za bei , kiasi cha fedha kilichotumika ni kikubwa kulingana na kazi iliyofanyika na kamati ya ujenzi kutoshirikishwa hatua za ujenzi huo kama mwongozo unavyoelekeza. Alisema uchunguzi umeanza ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wale waliohusika kukiuka mwongozo huo.

Alitaja ufuatiliaji mwingine kuwa ni wa mradi mkubwa wa ukarabati wa majengo ya shule ya Sekondari ya Morogoro, Manispaa ya Morogoro wa Sh 1,042,554,532. 80 ambapo ofisi yake ilibaini ukiukwaji mkubwa wa taratibu za mikataba katika eneo la zabuni, hivyo utangazaji zabuni hiyo ulifanywa upya. Alitaja mradi mwingine uliofuatiliwa ni ujenzi wa shule ya Sekondari Mji Mpya Manispaa ya Morogoro wa Sh bilioni 1.4 ambapo ilibainika kuwepo kwa ukiukwaji wa taratibu za manunuzi, ulipaji wa malipo ya awali ya kazi kinyume na taratibu na sheria za manunuzi na uingiaji wa mikataba usiofuata taratibu.

Alisema walifuatilia na kufanya uchunguzi juu ya matumizi ya fedha kiasi cha Sh bilioni 1.5 zilizotolewa na Serikali kuu kwa halmashauri ya wilaya ya Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo baada ya kubainika kuwepo kwa usimamizi usioridhishwa na mazingira ya rushwa kwenye ujenzi.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) , Selemani Jafo aliipa jukumu Takukuru mkoa la kufuatilia na kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha kiasi cha Sh bilioni 1.5 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa halmashauri ya wilaya ya Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.

Dk Kebwe alisema ujenzi huo umetumia Sh bilioni moja na majengo hayajafikia kupaua wakati taarifa ya halmashauri hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi huo ikionesha wamebakiwa ‘bakaa’ Sh milioni 400.

TATIZO sugu la mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi