loader
Picha

UDOM kuendelea na udahili Mlimani City

Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), kitaendelea kufanya Udahili jijini Dar es Salaam eneo la Mlimani City hadi Agosti 10 mwaka huu, baada ya kumalizika kwa Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo unayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Ushauri chuoni hapo, Profesa Alexander Makulilo alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo jijini Dar es Salaam.

Profesa Makulilo alisema, baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, UDOM wanahamia eneo la Mlimani City ambapo huko watakuwa wakiendelea na udahili kwa wanafunzi wanaotaka kuomba udahili.

Alisema chuo hicho ni chuo pekee nchini chenye program 147 ambazo ni idadi kubwa ukilinganisha na vyuo vingine.

Alisema mbali na kudahili wanafunzi wataendelea kutoa ushauri kwa mahitaji mbalimbali ya wale wanaotaka kujiunga.

Pia alisema wameshirikianana watoa huduma wengine wa elimu yajuu kuona ni jinsi gani wataboresha mitaala na kuvutia soko katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

UDOM ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mara moja na sasa wapo 30,000 wanataka kuongeza 10,000.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi