loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndalichako ataka umakini udahili vyuo vikuu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka viongozi wote wa vyuo vya elimu ya juu nchini kusimamia kwa ukaribu na umakini mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu yajuu kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa waombaji na wadau wengine wa elimu.

Ndalichako alitoa agizo hilo jana akifunga Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema anafahamu kuwa TCU imeshatoa maelekezo na mafunzo ya kutosha kwa wataalam wa mifumo ya kompyuta na maofisa udahili wa vyuo vyote vitakavyodahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2019/2020.

“Hivyo ni imani yangu kwamba kazi hii ya udahili itafanyika kwa ufanisi mkubwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita. Niwakumbushe kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania, jukumu la kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu ni la Seneti au Bodi ya chuo husika.

“Nawasihi viongozi wa vyuo mtumie mamlaka zenu za Seneti au Bodi ipasavyo katika kudahili wanafunzi wapya kwa mujibu wa Sheria na Miongozo iliyopo. Serikali haitasita kuchukua hatua kwa chuo chochote kitakachokiuka ama utaratibu wa udahili uliowekwa au kudahili wanafunzi wasiokidhi vigezo vya udahili,” alisema.

Aliwaasa pia wanafunzi wote watakaofanya maombi ya udahili kuwa makini katika kuchagua vyuo na programu kulingana na sifa zao, ili kuhakikisha wanapata nafasi katika vyuo vikuu.

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi