loader
Picha

Waziri aagiza wamiliki wa mialo watambulike

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amesema wanaomiliki mialo kwa ajili ya usafishaji wa madini lazima watambulike serikalini na watapatiwa eneo maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo kwani wanatumia zebaki kusafishia wakati wapo karibu na makazi ya watu.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama ambapo alieleza kuwa watakapotafutiwa eneo moja itaundwa kamati itakayosimamia na kuwawakilisha ili kuweza pia kuthibiti wizi unaoendelea kutokea kupitia mialo hiyo.

Waziri Biteko amesema amekuta mialo mingi iko kwenye uwanja katika kijiji cha Kakola tena karibu na makazi ya watu jambo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu kwani wanatumia mekyuri kusafisha kupata dhahabu na maji yanakwenda kwenye makazi.

“Mialo itawekwa kwenye eneo moja lazima wahamishwe haiwezekani watu wachenjue dhahabu kwa kutumia mekyuri kwenye makazi ya watu eneo lipo watajiunga kikundi cha watu takribani kumi kwa kutoa wawakilishi lakini uongozi huo lazima atakuwepo mwenyekiti wa kijiji, wanaotoka chama cha wachimbaji wadogo (Shirema) na wamiliki wa mialo,” alisema.

Waziri Biteko alimtaka kamishina wa madini mkoa wa Shinyanga Joseph Kumburu na mkuu wa wilaya ya Kahama Annamringi Macha kulisimamia upatikanaji wa eneo mara moja kwani ni lazima uwepo udhibiti kutokana na wizi uliokuwa ukifanyika.

TATIZO sugu la mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Kahama

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi