loader
Picha

'Chuma ulete' tatizo Rombo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameshtushwa na taarifa za imani za kishirikina wilayani Rombo na kuagiza wazee wa mila kutatua changamoto hiyo kuepuka kuwaogopesha watumishi wa umma huko.

Amesema mjini Same kuwa serikali haiamini mambo hayo lakini kuna umuhimu jambo hilo likatatuliwa kimila kinyume na hapo watumishi wa umma wataogopa kufanyakazi katika wilaya hiyo.

Kauli ya Majaliwa inafuatia taarifa ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira kwamba wananchi wa wilaya hiyo wana tatizo la upotevu wa fedha maarufu kama ‘chuma ulete’.

“Baadhi ya wafanyabiashara wa wilaya hii wanalalamikia kupotea kwa fedha ama kutopata faida na shughuli za kiuchumi wanazofanya, wanapata fedha lakini hawajui zinaishaje,” alisema Mghwira.

Alisema suala hilo linaweza kushughulikiwa na mbunge wa Same Magharibi, Dk Mathayo David, Mwenyekiti wa Halmashauri, Christopher Irira, Mwenyekiti CCM, Isaya Mngulu na wazee mashuhuri.

WATU 45 wamelazwa katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa wa ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Same

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi