loader
Picha

Rage- Kilomoni yupo sahihi

WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo Hamisi Kilomoni kwenye Kamati ya Midhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, achukuliwe hatua kwa kosa la kutumia kivuli cha udhamini kudhoofisha brand ya timu hiyo, suala hilo limemuibua mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Ismail Rage.

Rage amezishauri pande zote mbili kukutana na kumaliza tofauti zao na sio kuendelea kubishana kwenye vyombo vya habari, jambo ambalo si muharobaini wa kumaliza sintofahamu hiyo inayoendelea kila siku.

Ni muda mrefu sasa Simba imekuwa ikitunishiana misuli na Kilomoni jambo lilofanya uongozi wa wekundu hao kutoka hadharani na barua kutoka serikalini iliyoweka bayana kwamba Kilomoni sio mdhamini.

Akizungumza jana Rage alisema viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu Kilomoni ameitumikia timu hiyo toka inaitwa Sunderland si mtu mdogo wanapaswa kumuita kuongea naye.

“Sidhani kama kuendelea kubishana kila siku kwenye vyombo vya habari kunaweza kuleta suluhisho ni vyema uongozi wa Simba ukubali kukutana kuyajenga masuala haya kwa busara, “ amesema Rage.

Amesema Kilomoni hapaswi kujibiwa na Magori, kwa kuwa Magori ni mwajiriwa analipwa mshahara kama wafanyakazi wengine kinachotakiwa viongozi wa bodi wafanye mchakato wa kukutana kuweza kumaliza jambo hili.

“Unajua Kilomoni anachokidai ni cha msingi kabisa kutaka mwekezaji aweke kiasi cha bilioni 20 kwenye akaunti ndipo wapatiwe hati sasa tatizo liko wapi anachokidai ni sahihi wanatakiwa kufanya hivyo asikilizwe wayamalize,“ amesema Rage.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi