loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Afa kisa kucheza muziki kwenye joto kali Japan

KIJANA mmoja raia wa Japan amefariki dunia kwa joto baada ya kucheza muziki kwenye jua kwa dakika 20 akiwa amevaa mavazi ya ‘kikaragosi’ yaani ‘mascot costume’.

Inaelezwa kuwa mavazi hayo yalikuwa yana uzito wa kilogramu 16 na kutokana na joto kali linaloendelea kuongezeka nchini humo, kijana huyo alishindwa kustahimili kisha kupoteza maisha.

Kutokana na tukio hilo, lililotokea jijini Osaka, matumizi ya mavazi hayo yamepigwa marufuku katika kipindi hiki cha hali hiyo ya joto.

Kijana huyo ni moja ya watu 11 ambao wamefariki kutokana na joto na hadi sasa zaidi ya watu 5,000 wamekwenda hospitali kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayotokana na joto hilo.

Takriban asilimia 50 ya watu wote wanaopatiwa matibabu hayo ni wazee wa miaka 65 na zaidi, huku joto likitarajiwa kuendelea kuwa juu kwa wiki ijayo.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi