loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mhamasishaji Instagram akutwa amekufa kwenye sanduku la nguo

MHASISHAJI maarufu wa mtandao wa Instagram nchini Urusi, Ekaterina Karaglanova, 24, amekutwa amekufa kwenye sanduku la nguo nyumbani kwake.

Karaglanova ambaye alikuwa na wafuasi (followers) zaidi ya 85,000 Instagram alikuwa amehitimu hivi karibuni masomo yake ya udaktari.

Polisi wameeleza kuwa wanachunguza wivu kama sababu ya inayoweza kuwa imesababisha kifo cha binti huyo.

Mhamasishaji huyo alikuwa ameingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na alikuwa amepanga mapumzikoni huko Uholanzi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa jana, Julai 30.

Kwa mujibu wa wazazi wake, waliingiwa na hofu baada ya kuwa binti yao huyo hapatikani kwa simu, hivyo wakaenda hadi nyumba aliyokuwa amepanga na kumuomba mwenye nyumba afungue chumba chake.

Walikuta sanduku la nguo koridoni na walipolifungua wakamkuta binti yao akiwa na jeraha la kukatwa na kitu cha ncha kali shingoni akiwa tayari amefariki.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: MASHIRIKA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi