loader
Picha

SHELISHELI: Nchi iliyo katika 10 bora kwa utajiri Afrika

JAMHURI ya Shelisheli iliyo katika Bahari ya Hindi, ni moja ya nchi ndogo kwa eneo na idadi ya watu katika Afrika, lakini ni kati ya nchi 10 tajiri zaidi barani .

Ina ukubwa wa kilometa za mraba 451 zinazokaliwa na zaidi ya raia 94,000 katika visiwa 115.

Ongezeko la watu mwaka huu (2019) linatarajiwa kufanya idadi kufikia 97,739. Mwaka 2013 ilikuwa na nyumba za makazi zipatazo 192,993. Kisiwa hicho kilichopo katika ukanda wa kusini mashariki mwa Afrika, kaskazini mwa Madagascar, kabla ya kupata uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1976, historia inaonesha kiliwahi kukaliwa pia na Wafaransa, Wareno na Waarabu (kwa kilimo na biashara).

Wafaransa waliweka makazi ya kudumu baada ya Wareno na Waarabu miaka ya 1756 na ndio waliokipa jina kisiwa hicho na kukiita ‘Seychelles’ kwa heshima ya kiongozi wao wa wakati huo aliyeitwa Jean Moreau de Sechelles.

Katika Shelisheli, kisiwa kikubwa zaidi ni Mahe ambako ndiko mji mkuu wa nchi hiyo wa Victoria, ulipo. Wakazi wengi huishi huko na katika visiwa vya karibu ambavyo ni Praslin na La Digue. Jamhuri hiyo ina visiwa vyenye milima inayofikia mita 900.

Mlima mkubwa ni Morne Seychellois wenye mita 905. Hali ya hewa ni ya kitropiki (hali ya joto na nyakati za mvua). Mauritius na Shelisheli vilitawaliwa pamoja, lakini mwaka 1903 visiwa hivyo vilipewa cheo cha kila moja kuwa koloni.

Baada ya uhuru kulikuwa na vipindi vya kubalidilisha katiba ikiwemo mabadiliko yaliyodumu mpaka sasa ya mwaka 1993 yaliyorasimisha mfumo wa vyama vingi nchini humo kutoka katika chama kimoja yaliratibiwa mwaka 1991 chini ya chama tawala cha Seychelles People’s Progressive Front (SPPF).

Katiba ya nchi hiyo imeweka vipindi vya uongozi vya miaka mitano na rais ndiye mkuu wa nchi. Raisi wa sasa ni Danny Faure aliwahi kuwa Makamu wa raisi wa nchi hiyo.

Ripoti ya uchumi ya Shirika la Fedha Duniani (IFM) inaeleza kuwa Pato la Taifa mwaka jana lilikuwa Dola za Marekani bilioni 1.59, ikiwakilisha chini ya asilimia 0.01 ya uchumi wa dunia. Sekta ya utalii ndio tegemeo kubwa la uchumi wa nchi hiyo.

Inachangia takriban asilimia 70 katika pato la taifa kwa takwimu za mwaka 2018. Sekta hiyo inaajiri zaidi ya asilimia 30 ya wananchi.

Utalii mkubwa pia unafanyika katika fukwe za kuvutia za nchi hiyo na mbuga za wanyama. Kilimo kikuu kinahusu mazao ya biashara kama chai, viazi mbatata, viazi vitamu, mihogo na nazi na kinachangia zaidi ya asilimia mbili.

Uvuvi wa samaki aina ya jodari huwezesha uwepo wa viwanda vya samaki na kusindika mazao. Kwa mara ya kwanza Shelisheli ilijiunga na SADC Septemba mwaka 1997 hadi Julai mwaka 2004 na kisha ikajiunga tena mwaka 2008.

 

Kwa kipindi kirefu kumekuwa na mikakati ya kuongeza pato la ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi