loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa- Tuna sukari ya kutosha

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Tanzania haina shida ya sukari kwa sababu inayozalishwa ndani ya nchi ipo na inatosha.

Majaliwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda kwenye Maonesho ya Nne ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais John Magufuli alizindua maonesho hayo jana.

Kwa mujibu wa Majaliwa, sukari ya Tanzania inazalishwa kwenye viwanda vilivyopo Tanzania bara na Zanzibar.

"Tuna fursa pia ya kukaribisha viwanda kutoka nje ya nchi kuja kwekeza hapa Tanzania. Moja ya wito wetu sisi kama Serikali na sisi kama Watanzania ni ujenzi wa viwanda. Mataifa yote haya ya nje yaliyokuja hapa yameleta bidhaa zao...

" tunayo fursa ya wao kuja kuzalishia hapa kwetu, kuungana na Watanzania wenye ardhi, wenye mtaji ambao wanaweza kuunganisha na mtaji wa wageni wetu wakaanzisha kiwanda na kupanua wigo" amesema.

Ametoa mwito kwa Watanzania kutembelea maonesho hayo ili waweze kutambua nani anataka kuja kuwekeza Tanzania ili waunganishe nguvu wajenge kiwanda chenye mtaji mkubwa, wazalishe bidhaa na kusaidiana kupanua wigo wa masoko.

Majaliwa pia ametoa mwito kwa wafanyabiashara nchini kuziuza na kuzitambulisha vizuri bidhaa zao ili zipate masoko ndani ya nchi wanachama wa SADC na kwingineko.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi wanachama SADC yamekamilika kwa kiasi kikubwa na tayari kuna ratiba ya uingiaji wageni.

Ametoa mwito kwa Watanzania kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vyote vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini.

"Sisi Watanzania tunayo sifa na heshima ya ukarimu.Tutumie nafasi hii sasa kuonyesha kwa kuwakaribisha wageni wetu, waingie nchini, wakae katika kipindi chote na warudi wakiwa salama lakini warudi wakiwa wamerudi na ujumbe wa ukarimu ambao tunao" amesema.

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi