loader
Picha

CRDB yapata faida bil 86.65/-

BENKI ya CRDB imepata faida ya Sh bilioni 86.65 kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ikiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 98 kutoka Sh bilioni 43.85 iliyoipata kipindi hicho mwaka uliopita.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela amesema jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko la faida hiyo limetokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara na jitihada binafsi za benki.

Nsekela amesema katika kipindi cha mwaka huu, benki hiyo imepata mafanikio hayo yaliyotokana na mapato kuongezeka hali iliyotokana na kuimarika kwa mapato halisi ya riba na mapato halisi yasiyo ya riba sambamba na kuongeza kiwango cha mikopo huku wakishusha uwiano wa mikopo chechefu.

“Mikopo tuliyotoa kwa wateja iliongezeka sambamba na amana za wateja huku tukiwafikia wateja wapya kupitia huduma za kidijitali kama vile SimBanking, SIMAccount na mawakala wetu wa CRDB nchini,” amesema Nsekela.

Alisema mafanikio mengine yaliyosaidia kuifikisha hapo imetokana na kuongezeka kwa pato litokanalo na ubadilishaji wa fedha za kigeni ambalo katika kipindi cha hivi karibuni idadi kubwa ya wananchi, taasisi za kigeni na watu binafsi wamejitokeza kwa wingi katika matawi yao kubadilisha fedha.

 TANGU mwishoni mwa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi