loader
Picha

Tanzanite yatinga fainali Cosafa

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite jana ilitinga fainali za michuano ya Kombe la Cosafa na sasa itacheza na Zambia keshokutwa.

Tanzanite ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Afrika Kusini katika mechi ya nusu fainali ya pili, huku wapinzani wao, Zambia wakiifunga Zimbabwe mabao 4-0 katika nusu fainali ya kwanza.

Michezo yote hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Gelvandale Port Elizabeth, Afrika Kusini. Katika mchezo, huo ushindi wa Tanzanaite ulipatakana kupitia mabao ya Enekia Kasonga dakika ya 18 na bao la pili likiwekwa kimiani na mwanadada Opa Sanga dakika ya 22.

Mechi ya fainali inatarajiwa kuwa ya kisasi kwani Tanzanite na Zambia zilikuwa kundi moja na katika mechi yao, Zambia iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mbali na mechi hiyo, lakini Tanzania na Zambia zilishakutana kwenye michuano kadhaa na mara zote Zambia imekuwa ikitamba.

Tuzo Mapunda SIMBA imeanza vyema msimu huu baada ya kuifunga ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi