loader
Picha

Biashara nayo yaja na tamasha

UONGOZI wa timu ya Biashara United umeanzisha Wiki ya Biashara inayojulikana kama Biashara Family Week iliyoanza juzi na kilele chake kinatarajiwa kuwa Jumapili ya wiki hii kwa mchezo wa kimataifa dhidi ya Tusker ya Kenya.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Sulemani Mataso alisema jana lengo la kuanzisha tamasha hilo ni kurudisha fadhila kwa mashabiki wa timu hiyo walioisapoti timu hadi kubakia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema kupitia tamasha hilo, watatangaza kikosi watakachokuwa nacho msimu ujao wa ligi na kutambulisha wachezaji waliosajiliwa.

“Pamoja na kurejesha shukrani kwa mashabiki, lakini pia kupitia mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, timu itapata maandalizi mazuri kwa ajili ya Ligi Kuu,” alisema Mataso.

Alisema kupitia wiki hiyo wanachama na wakereketwa wa timu hiyo, wanafanya shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi kwenye vituo vya Afya, na kutoa misaada kadhaa.

Biashara inakuwa miongoni mwa timu zilizofuata nyayo za Simba kuwa na wiki yake ambapo wachezaji, wanachama na mashabiki wake hufanya shughuli za kijamii kisha kuadhimisha kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa ambapo hutambulisha kikosi kipya, wengine waliofanya hivyo ni Ndanda miaka ya nyuma na mwaka huu, Yanga imefanya hivyo mwishoni mwa wiki.

TIMU ya Tanzania Bara ya wasichana walio chini ya Umri ...

foto
Mwandishi: Na Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi