loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viwanda 54 kutumia gesi

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) litaongeza viwanda vinavyotumia gesi asilia ndani ya miaka mitatu kwa kuunganisha viwanda 10 viwe 54 vinavyotumia kupunguza gharama za uzalishaji.

Kwa sasa viwanda 44 vinatumia gesi asilia ambayo ni nishati nafuu kuokoa gharama ya matumizi kwa asilimia 50 hivyo uzalishaji bidhaa kuwa nafuu na wananchi kupata kwa urahisi na gharama nafuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, James Mataragio alisema hayo alipotembelea viwanda vinavyotumia gesi asilia katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Mataragio na maofisa wa TPDC walitembelea viwanda vitatu vya Goodwill kinachozalisha vigae (Tiles) kinachotumia gesi kwa miaka mitatu, Lodhia Still kinachotengeneza nondo kinachotumia gesi miezi miwili, na Knauf kinachotengeneza jasi kinachoendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuingiza gesi.

Mataragio alisema baada ya kutembelea viwanda hivyo na kuona miundombinu ya gesi asilia wawekezaji wamemweleza kuwa wamefurahi kuokoa gharama kwa kutumia gesi asilia na kuwaalika wawekezaji zaidi kuunganisha gesi asilia kwani miundombinu ipo tayari na kuna gesi ya kutosha.

Alisema viwanda 44 vinavyotumia gesi futi za ujazo zaidi ya milioni 39 vipo Mtwara, Dar es Salaam na Pwani vingine vikiwa hatua mbalimbali za kuingiziwa gesi hivyo wamejiwekea lengo miaka mitatu ijayo kuunganishia viwanda 10.

Meneja Uzalishaji Goodwill alisema miaka mitatu waliyotumia gesi asilia hawajawahi kukosa nishati ya umeme kwa kufanya uzalishaji kila siku wakitengeneza vigae vya mita za mraba 40,000 kwa siku.

Alisema hawajawahi kutumia nishati nyingine bali gesi asilia ambayo haina changamoto za kukatika.

Meneja Mkuu Lodhia, Raju Singh alisema awali walikuwa wakizalisha bidhaa kutumia makaa ya mawe lakini wana miezi miwili wanatumia gesi asilia hivyo kuokoa gharama na kuwa rafiki wa mazingira.

Alisema wamekuwa wakitumia Sh milioni 250 kwa mwezi lakini sasa gesi asilia wanatumia Sh milioni 80 pekee .

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi