loader
Picha

Malighafi chache kikwazo uchumi Afrika

Nchi wanachama wa Jumaiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) bado zinakabidiliwa na changamoto ya kuagiza malighafi nyingi zaidi kutoka nje ya Afrika.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda na Biashara wa Sekretarieti ya SADC Calicious Tutalife, ameyasema hayo alipozungumza na Daily News Digital, jijini Dar es Salaam.

Tutalife amesema, Waafrika wengi wanadhani kuwa nchi za Afrika hazifanyi biashara baina yao vya kutosha kwa sababu usindikaji unafanywa nje ya bara jambo analosema halina ukweli.

“Ukweli ni kwamba kama bara, mazao tunayozalisha hayatoshi kukidhi mahitaji yetu, ndio maana tunanunua mazao kutoka nje ya Afrika, japokuwa na sisi tunazalisha mazao hayo hayo,” ameongeza.

Ametoa mfano wa mazao yanayozalishwa kwa uchache ni soya ambayo huzalishwa hadi tani moja kwa mwaka huku mahitaji ya zao hilo yakiwa tani tatu.

Mazao mengine ni mchele, ngano, mahindi pamoja na pamba ambayo japokuwa yanazalishwa na nchi hizo za SADC ikiwa ni pamoja na Tanzania, bado yanabaki kuwa chini ya asilimia 50 ya uhitaji uliopo.

“Kinachotakiwa kufanyika ni kuzalisha zaidi huku miundombinu ya usafiri ikiboreshwa ili kuwepo na usafirishwaji bora na wa kutosha wa mazao baina ya nchi washiriki,” amesema.

SERIKALI imejizatiti kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa ukienda sanjari ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi