loader
Picha

SADC yajivunia umeme maporomoko Rufiji

KURUGENZI ya Miundombinu na Huduma ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imesema inajivunia mradi wa kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Mwalimu Julius Nyerere) kutokana na manufaa yake kwa nchi wanachama.

Aidha, imeipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa miradi ya kisekta ya miundombinu ambayo pamoja na kuipaisha Tanzania kiuchumi, pia ina manufaa makubwa kwa nchi za SADC na Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa Sekretarieti ya SADC, Mapolao Mokoena alimpongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake na kuhakikisha mradi huo unatekelezwa.

Mokoena alisema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya yeye pamoja na wakurugenzi wengine kuwasilisha mada kuelezea shughuli na malengo ya kurugenzi mbalimbali ndani ya sekretarieti ya SADC.

Miongoni mwa maswali hayo lilitaka kupata maoni yake juu ya mradi mkubwa wa kuzalisha umeme uliozinduliwa hivi karibuni Rufiji, mkoani Pwani, nchini Tanzania na Rais Magufuli.

“Tunajivunia huu mradi,” alisema na kuongeza kuwa mradi huo una manufaa si tu kwa nchi za SADC bali pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Bara zima.

Rais Magufuli alizindua mradi huo mkubwa wa uzalishaji umeme Julai mwaka huu, ukitarajiwa kuwezesha nchi kupata umeme wa kutosha. Unatarajiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme na Ujenzi wa bwawa hilo unaofanywa na wakandarasi kutoka Misri unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 2.9; takribani Sh trilioni 6.5.

Awali, akiwasilisha mada kuhusu maendeleo ya miundombinu na huduma ndani ya SADC kwenye eneo la nishati, alisema Mpango Kazi wa Maendeleo ya Miundombinu (RIDMP) wa mwaka 2012-2027 unalenga kuhakikisha kunakuwa na usalama wa rasilimali ya nishati na uhakika wa upatikanaji wake kama injini ya kuinua uchumi.

Alitaja eneo muhimu linalopewa kipaumbele na kutazamwa kiuchumi zaidi katika nishati kuwa ni upatikanaji na ugunduzi wa gesi na mafuta katika nchi wanachama na namna nchi hizo zinavyotumia nishati hizo kupata uhakika wa umeme kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi na Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi