loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ramaphosa wa kwanza kuwasili kwa SADC

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa atawasili nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli leo.

Rais Ramaphosa atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili pamoja na kuhudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungumza jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema Rais Ramaphosa atawasili nchini saa tano usiku, na baada ya ziara hiyo ataendelea kuwepo nchini kusubiri kilele cha Mkutano wa SADC.

Makonda alisema Marais wengine watawasili nchini Agosti 16 na alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuwa karibu na vyombo vya habari kusikiliza matangazo mbalimbali ya maelekezo kutoka kwa vyombo husika kwani baadhi ya barabara zitafungwa.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi