loader
Picha

EAC yaguswa ajali ya moto, yamfariji Magufuli

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imeguswa na ajali ya mlipuko wa lori la mafuta uliosababisha vifo vya watu 75 na kujeruhi wengine, huku ikisema ina cha kujifunza hasa katika wakati huu ambao nchi za EAC zinaingia katika biashara ya mafuta baada ya kugundulika kwa nishati hiyo katika nchi zao.

Kwa sasa, Kenya, Sudan Kusini na Uganda zina utajiri mkubwa wa mafuta, huku Tanzania yenye utajiri wa gesi kuliko zote katika Afrika Mashariki, Rwanda na Burundi zikifanya utafiti katika maeneo mbalimbali.

Ujumbe huo wa EAC umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa EAC, Steven Mlote katika salamu zake za rambirambi kwa Rais John Magufuli, jana jijini Arusha. Alisema EAC imeguswa na vifo na majeruhi wa ajali hiyo, hivyo inaungana na ndugu, jamaa na marafiki wa watu walioathirika kutokana na ajali hiyo Jumamosi ya Oktoba 10, mwaka huu katika eneo la Msamvu-Itigi, mjini Morogoro.

“Ni msiba mkubwa sana. Tunaungana na Rais John Magufuli na Watanzania wote katika kuomboleza msiba na pia kuwatakia nafuu ya haraka wote walionusurika katika ajali ya Morogoro,” ilisema sehemu ya taarifa ya Mlote.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi