loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiwanda cha kukausha matunda kuingia soko SADC

KIWANDA cha kukausha matunda na viungo cha kampuni ya ELVEN Agri Co Limited kimepanga kuingia katika soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanya biashara kwa kiwango cha juu.

Kiwanda hicho kinachofanya biashara hivi sasa katika baadhi ya nchi za SADC ikiwamo Tanzania, Zambia na Botswana, soko lake kubwa lipo Japan, Australia na nchi za Ulaya.

Meneja wa Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Brij Kumari, alisema lengo la kiwanda ni kushirikiana na serikali kuzalisha ajira, chakula bora na kufanya biashara yenye viwango katika nchi mbalimbali. Alikuwa akiwasilisha mada kwa ujumbe wa SADC; ambao walikuwa washiriki wa maonesho ya nne ya viwanda yaliyohitimishwa wiki iliyopita.

Washiriki hao kutoka nchi 16 za jumuiya, walitembelea viwanda mbalimbali kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua katika kutekeleza sera ya viwanda.

“Sasa hivi kutokana na hamasa tunayoipata kutoka serikalini, tumejipanga kupeleka bidhaa zetu katika nchi za SADC, tunaomba ushirikiano wenu kupata ushauri na mawazo mapya ili tuweze kuifikia lengo kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kumari.

HUDUMA za Afya Aga Khan Tanzania na Shirika la Maendeleo ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi