loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bei ya vyakula yaleta unafuu wa maisha

TAKWIMU za utafiti uliofanywa na gazeti la New Times la nchini hapa katika masoko mbalimbali zinaonesha kuwa kuna ongezeko la bei za chakula ingawa bado ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2017 na nusu ya pili ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa takwimu, kilo ya viazi mbatata inakadiriwa kuwa kati ya Faranga 240 na Faranga 290 ukilinganisha na Septemba mwaka jana na 2017 ambapo ilikuwa zaidi ya Faranga 290.

Imeelezwa ni sawa na bei ya mihogo na ndizi ambayo inakadiriwa kuwa Faranga 150 na Faranga 200 kwa sasa ni kati ya Faranga 140 na 190. Baadhi ya sababu za kupungua kwa bei hiyo zilizotolewa na wafanyabiashara ni serikali kwa sasa kuingia kati udhibiti wa bei kulingana na soko.

Mfanyabiashara wa viazi mbatata, Theoneste Nzanimpa, alisema mikakati iliyofanywa ya kuondoa watu wa kati waliotumika kuongeza bei kutoka kwa wakulima kwenda kwa walaji imesaidia kurekebisha kudhibiti hali.

Alisema wamekuwa wakipongeza bei kwa zaidi ya faranga 60 kwa kilo, hivyo kutokana na serikali kuingilia kati, wakulima sasa wanauza moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaouza kwa watumiaji wa mwisho.

Mkurugenzi Mkuu wa Utafiti wa Kilimo na Teknolojia katika Bodi ya Maendeleo ya Kilimo na Rasilimali za Wanyama Rwanda, Dk Charles Bucagu, alisema mbali na kufanya mabadiliko sokoni, serikali kupitia wizara ya kilimo na taasisi zilizo chini yake imekuja na mikakati ya kuangalia hali ya hewa na kuthibiti magonjwa hivyo kuongeza mazao.

WILAYA tatu za mkoa wa Lindi za Nachingwea, Ruangwa na ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi