loader
Picha

Sare zatawala timu za EAC

SARE zinaonekana kutawala katika mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa na zile za Shirikisho Afrika kwa klabu za Afrika Mashariki, baada ya mechi za ufunguzi wa msimu huu wikiendi iliyopita.

Kwa michuano yote hiyo miwili, jumla ya sare saba zimepatikana kutoka jumla ya mechi 12 zilizochezwa za Ligi ya Mabingwa Afrika na zile ya Kombe la Shirikisho.

Jumla ya sare nne za bila kufungana huku kukiwa na sare mbili ambazo timu zimefungana kwa kutoka sare ya bao 1-1, ambazo ni Yanga ilivutwa shati na Township Rollers ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa katika Ligi ya Mabingwa, huku Rayon Sports ya Rwanda nayo ilitoka sare kama hiyo dhidi ya Al Hilah ya Sudan.

Kwa matokeo ya suluhu, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba, wenyewe waliilazimisha sare ugenini dhidi ya UD Songo ya Beira, Msumbiji huku Aiger Noir ya Burundi ikitoka sare dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mchezo uliofanyika Burundi.

Suluhu nyingine zilipatikana kutoka katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika wakati timu ya Mogadishu City ya Somalia dhidi ya Malindi ya Zanzibar katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, wakati KMC ikilazimisha sare ugenini dhidi ya AS Kigali ya Rwanda.

Timu zilizopoteza kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki ni KCCA ya Uganda baada ya kufungwa 3-2 na African Stars ya Namibia katika Ligi ya Mabingwa na Lukinzo FC ya Burundi ilipofungwa mkono (5-0) dhidi ya Triangle United ya Zimbabwe na Azam ya Tanzania Bara ilifungwa 1-0 dhidi ya Fasil Ketema ya Ethiopia zote Kombe la Shirikisho.

Katika ukanda huo wa Afrika Mashariki timu pekee iliyoshinda mwishoni mwa wiki ni ile ya Proline FC ya Uganda baada ya kuibuka na mabao 3-0 dhidi ya Master Security ya Malawi katika mchezo uliochezwa Uganda.

Kutokana na matokeo hayo, jumla ya mabao saba yalifungwa na timu hizo, huku wakifungwa 13 katika jumla ya mechi 12 za raundi ya awali za michuano hiyo miwili mikubwa ya klabu barani Afrika.

Kwa hiyo, matokeo hayo yanadhihirisha kuwa timu nyingi katika ukanda wa Afrika Mashariki zilikuwa na safu butu ya ushambuliaji, hivyo zinahitaji kujiimarisha zaidi ili ziweze kutinga raundi inayofuata.

Pamoja na uwingi wa timu za Afrika Mashariki huenda zikaanza kupungua katika raundi inayofuata na nyingi kushindwa kufuzu kwa hatua ya makundi ya mashindano hayo ya Afrika.

Ni wazi timu hizo zinahitaji kufanya maboresho kwenye safu ya ushambuliaji na changamoto nyingine ndogondogo zilizojitokeza kwenye michezo yao ya awali kama wanahitaji kuendelea kufanya vizuri.

Mechi za marudiano za Ligi ya Mabingwa na zile za Shirikisho la Afrika, zinatakuwa kupigwa wiki mbili zijazo, kati ya Agosti 23 hadi 25, ambapo washindi wa jumla kwa mechi zote mbili, watasonga mbele.

Katika msimu ulioita Simba ilifikia hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa wa Afrika wakati Gor Mahia ilitolewa katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika huku KCCA walitolewa hatua ya makundi.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi