loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malindi wajipanga kuwamaliza Wasomali

KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya Malindi, Ahmed Saleh Machupa amesema matokeo ya sare waliyoyapata wakiwa ugenini sio mabaya na wanajipanga kuhakikisha wanashinda katika mechi yao ya nyumbani.

Malindi ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika ilishuka uwanjani katika dimba la Amaan kucheza na Mogadishu City ya Somalia ambao walikuwa ugenini baada ya wapinzani wao hao kuomba kuutumia kutokana na kwao Somalia kutokuwa na usalama.

Machupa amesema mchezo huo pamoja na kuwa ulichezwa katika uwanja wake wa nyumbani, lakini kiuhalisia wao ni wageni na wachezaji wake walicheza kwa umakini mkubwa kwa kuhofia kufungwa.

Hivyo alisema kuwa katika mchezo unaofuata, ambao Malindi watakuwa nyumbani, wamepania kushinda ili kusonga mbele hatua inayofuata.

Aidha alisema kuwa kupitia mchezo wao wa juzi wamebaini udhaifu kwao na kwa wapinzani wao, hivyo wataufanyia kazi kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo.

“Wapinzani wetu udhaifu wao tumeuona na sisi tumeonesha udhaifu wetu, lakini tunaondoka hapa na kwenda kuyafanyia marekebisho,” alisema.

Kwa upande wake kocha wa Mogadishu City, Mohammed Mistri Lamjed amesema kuwa walicheza kwa tahadhari sana ili kuhakikisha hawapotezi mchezo huo.

Alisema mechi hiyo kwao ilikuwa ngumu sana kutokana na kwamba walicheza wakiwa ugenini ingawa walikuwa wao ni wenyeji wa mchezo huo.

Katika mchezo wao wa awali miamba hiyo ilifanikiwa kutoka na sare isiyokuwa na mabao ambapo kila mmoja anahitaji ushindi wa angalau kuanzia bao 1-0 ili iweze kusonga mbele.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi