loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zanzibar watuma rambirambi vifo Morogoro

KAMATI ya Maafa ya Kitaifa ya Zanzibar imemtumia salama za rambirambi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutokana na vifo vya wananchi vilivyotokea Msamvu mkoani Morogoro kwa ajali ya mlipuko wa gari la kubeba mafuta mwishoni mwa wiki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maafa ya Zanzibar ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi alisema ajali ya mlipuko wa gari hilo la mafuta ni kubwa iliyoua wananchi kwa wakati mmoja.

Alisema wananchi wa Zanzibar wameguswa na taarifa ya ajali hiyo kwa sababu Watanzania ni ndugu.

“Huu ni msiba mkubwa ambao umewafika wananchi wenzetu wa Morogoro...nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maafa natoa salamu za pole,” alisema Balozi Idd katika salamu zake za pole juzi.

Aliwataka ndugu na jamaa wa watu mbalimbali waliofikwa na msiba huo mkubwa kuwa watulivu huku akiwaombea majeruhi kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.

Aidha Balozi Iddi alitoa nasaha zake na kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuacha kukimbia wakati majanga au ajali zinazotokea zaidi zinazohusu gari zinazobeba mafuta ya petroli ambayo ni hatari.

Alisema siku zote watu wajenge tabia ya kutoa taarifa wakati yanapotokea majanga au ajali na si kukimbilia moja kwa moja kama ilivyotokea katika eneo la tukio la ajali. Watu 71 wamefariki dunia katika ajali hiyo huku majeruhi 43 wakisafirishwa na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam.

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vyombo ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi