loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benjamin Mkapa kuzibua mishipa ya moyo

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH), Dodoma imeanza kufanya uzibuaji wa mishipa iliyoziba kwenye moyo.

Huduma hiyo itatolewa kwa mgonjwa mwenye tatizo kwa kutofanya upasuaji ila kutumia teknolojia ya kisasa ya ‘bomba nyembamba’ linaloenda kuzibua au kufungua mishipa ya damu kwenye moyo.

Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Moyo katika hospitali hiyo, Dk Wilfredius Rutahoile amesema kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji huo kwa mgonjwa aliyekuwa na matatizo ya kuziba kwa mishipa, hatua inayofanya hospitali hiyo kuwa ya kwanza nje ya hospitali za Dar es Salaam kutoa matibabu hayo.

“Watu wenye shida ya atherosclerosis (mirija au mishipa kwenye moyo) Dodoma na mikoa mingine wanaweza kupata matibabu Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Awali watu wenye matatizo kama haya nchi nzima walilazimika kusafiri hadi Dar es Salaam kupata matibabu kwa sasa hilo limerahisishwa,” alisema.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Kambi alitembelea hospitali hiyo wiki iliyopita baada ya wataalamu wake kufanya upasuaji wa kwanza wa kuzibua mishipa ya moyo kwa mgonjwa wa kwanza.

Profesa Kambi alitumia tukio hilo kuwapongeza madaktari kwa mafanikio makubwa waliyoyafikia. Dk Rutahoile alisema watu watano wenye matatizo ya mishipa ya moyo wamepatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, takribani wiki moja tangu hospitali hiyo kuanza kutoa huduma hiyo.

“Wakati mmoja wa wagonjwa watano wenye shida ya kuziba kwa mirija au mishipa ya damu kwenye moyo akiwafanyia upasuaji, wengine wanne walipewa dawa na kuwa chini ya uangalizi,” amesema.

Dk Rutahoile amesema matibabu ya kuzibua mishipa ya damu yanaimari- sha mtiririko wa damu kwenye moyo jambo linalopunguza maumivu ya kifua yanayotokana na matatizo ya kuziba kwa mishipa ya moyo.

Amesema katika upasuaji wa mgonjwa wa kwanza, madaktari wa magonjwa ya moyo Hospitali ya Benjamin Mkapa walishirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (TCS) kufanya upasuaji.

Rais wa TCS, Dk Robert Mvungi amesema madaktari wa moyo TCS walishirikiana na wa BMH wakati wa uchunguzi na utoaji matibabu kwa wenye matatizo ya kuziba mishipa ya moyo kambi ya wiki mbili.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi