loader
Picha

Rais Ramaphosa kwenda Morogoro

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili nchini kesho, Jumatano kufanya ziara na kushiriki mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dk Hassan Abassi amesema, kiongozi huyo atawasili kesho jioni.

Dk. Abassi amesema, Rais Ramaphosa atafanya ziara ya kikazi na kisha atahudhuria mkutano huo Agosti 17 na 18.

“Katika ziara yake hiyo atatembelea eneo la Mazimbu, mkoani Morogoro, sehemu ambapo wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika ikiwemo Afrika Kusini walipewa hifadhi wakati wa harakati wa nchi hizo,” amesema Dk Abbasi.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hadi sasa nchi zote 16 zimethibitisha kushiriki kwenye mkutano huo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Leo Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri SADC na ataifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja.

Wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali Rais John Magufuli atakabidhiwa jukumu la kuiongoza jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi