loader
Picha

Kijana afariki dunia akizini na mjane shambani

Kijana mwenye umri wa miaka 35 amefariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye shamba la mahindi na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mjane.

Polisi wamemtaja kijana huyo kuwa ni Julius Bor na kwamba, ameaga dunia jana usiku shambani kwenye eneo la Kapsaret katika Kaunti Uasin Gishu nchini Kenya.

Imefahamika kwamba, kabla ya tukio hilo, Julius alikuwa baa usiku kwenye Kituo cha biashara cha Chepyakwai akinywa pombe na mpenzi wake aliyetajwa kwa jina la Janet Misik Cheruto anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 50.

Inadaiwa kuwa, wapenzi hao walikuwa hapo hadi usiku wa manane na waliondoka pamoja.

Kwa mujibu wa Polisi, Julius na Janet walikwenda shambani kufanya mapenzi na wakati wakiendelea na tendo hilo mwanaume huyo alipoteza fahamu na akafariki dunia.

Inadaiwa kuwa, Janet amewaeleza Polisi kwenye eneo la tukio namna Julius alivyokuwa akihitaji kufanya mapenzi bila kupumzika baada ya kumeza dawa za kuongeza nguvu za kiume.

Janet anadaiwa kuwaeleza wapelelezi kuwa, wakati wakienda nyumbani Julius alikosa uvumilivu akahitaji wafanye mapenzi kwenye shamba la mahindi lakini wakati wakiendelea alianza kuumwa na akafariki dunia.

Polisi wamesema, baada ya Julius kupoteza fahamu, Janet alikimbia kwenda kumchukulia maji ya kunywa na aliporudi alimkuta bado hajitambui.

Janet alikwenda kutoa taarifa kwa mzee wa kijiji ambaye alitoa taarifa Kituo cha Polisi Kiambaa.

Mwili wa Julius umekutwa kwenye shamba la mahindi bila jeraha lolote na umepelewa chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Moi, Eldoret kwa ajili ya uchunguzi.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi