loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makonda- Wasanii tumieni fursa mkutano SADC

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa mwito kwa wachoraji picha na wachonga vinyago wautumie mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuonesha kazi zao za sanaa.

Makonda ametoa mwito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wasanii hao.

Amesema, ni muhimu kwa Watanzania waendeleze utamaduni wa kupenda vitu vya nyumbani kwa kuwa vinaongeza thamani na kuwatambulisha.

“Nimeona nitumie fursa hii kuwaomba Watanzania kutambua utamaduni wetu na kuvifahamu vitu vyetu kwa sababu ndio unaoleta thamani unapojua ulichonacho,” amesema.

Amesema, mkoa umewaandalia wachonga vinyago na wachora picha eneo la Samora Avenue, Wilaya ya Ilala ili wageni wanaokuja nchini kwa ajili ya mkutano huo waende huko kuona ubunifu wa wasanii wa Tanzania.

Makonda amesema, wachongaji na wachoraji kutoka Mwenge, Msasani na maeneo mengine ya jiji hilo waende maeneo ya Posta barabara ya Samora kufanya biashara.

“Kuna baadhi ya picha tunazinunua kutoka nje ya Tanzania, lakini kumbe zimetengenezwa hapa hapa Tanzania,” amesema.

Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC unatarajiwa kufanyika Dar es Salaam Agosti 17 na 18 mwaka huu.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi