loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JK: Magufuli anachukua uenyekiti SADCTanzania ikiwa mpya

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amefi chua siri ya namna Tanzania ilivyokabidhiwa kijiti cha kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) mwaka 2003 kibahatibahati na namna ilivyoandaa mkutano katika mazingira magumu.

Amesema mazingira ya wakati huo ni tofauti na mazingira ya sasa, ambapo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa SADC ikiwa mpya kutokana na kuwa na mazingira bora ya miundombinu ya kumbi za kimataifa za mikutano na hoteli nyingi za hadhi ya juu. Wakati mkutano huo unafanyika nchini mwaka 2003, Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Akilinganisha mazingira ya wakati huo na sasa, Kikwete alisema mwaka huu Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa SADC ikiwa ni nchi mpya kutokana na kuwa na mazingira bora zaidi ya kumbi za mikutano na hoteli zikiwa nyingi zaidi ya ilivyokuwa wakati ule.

“Hivi sasa unachagua tu ufanye mkutano katika ukumbi gani. Unaweza kuamua kuufanyia pale Mwalimu Nyerere International Convention Center au hata pale Ikulu, kuna ukumbi mzuri mkubwa tu, kwa hiyo chaguo ni lako,” alisema Kikwete.

Alitoboa siri hiyo wakati wa mahojiano maalum baina yake na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ambao ni wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL) jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia namna Tanzania ilivyopata Uenyekiti wa SADC mwaka huo, Kikwete alisema awali Zimbabwe ndiyo iliyokuwa iwe mwenyeji wa mkutano wa mwaka huo, lakini viongozi walibatilisha uenyeji wake katika dakika za mwisho kutokana na kudorora kwa uhusiano wa Rais wa Zimbabwe wa wakati huo, Robert Mugabe na jumuiya ya kimataifa.

“Ilikuwa iwe zamu ya Zimbabwe kuwa mwenyekiti wa mkutano, lakini wale viongozi wa SADC wanaoratibu zile zamu za nchi kuwa mwenyeji wa mkutano walipofika katika kipengele hicho waliitana wakajadili na kuamua kuwa isingekuwa busara kuipatia Zimbabwe uenyeji wa mkutano wakati ikiwa katika hali mbaya ya uhusiano na jumuiya ya kimataifa.

“Ndio sasa wakati wakiendelea kutafuta ni nani awe mwenyeji wakabaini kuwa kuna nchi ambayo ilikuwa haijawahi kabisa kuandaa mkutano wa SADC ambayo ni Tanzania. Wakaniita mimi wakaniambia sasa ni zamu yenu kuandaa maana haiwezekani kila siku nyie mnakula tu bila nyie kuliwa… (kicheko).

“Basi nilipoambiwa hilo nikampigia simu Rais Mkapa, nikamwambia hawa wakubwa wameamua mkutano ujao wa Sadc ufanyike nchini kwetu na bila kusita naye akakubali, ndio ukawa mwanzo wa sisi kuanza kuandaa mkutano ule,” alisema Kikwete.

Alisema hata hivyo jukumu hilo la kuandaa mkutano huo, liliwaweka katika wakati mgumu viongozi wa serikali, baada ya kuibuka kwa sintofahamu ya wapi mkutano huo ufanyike kutokana na ukosefu wa kumbi za kimataifa za mikutano katika Jiji la Dar es Salaam, ambako kulikuwa na hoteli za hadhi nzuri za kuwaweka wajumbe wa mkutano huo.

“Hili suala lilituumiza sana kichwa, Kwa Dar es Salaam changamoto tuliyokumbana nayo wakati ule ilikuwa ni kwamba hoteli zipo za kutosha lakini hatuna ukumbi wa mikutano wenye hadhi ya kuchukua wajumbe wengi wa SADC, tukapata wazo tupeleke Arusha maana pale kuna kumbi za mikutano za kimataifa, lakini tukakwama maana wao hawakuwa na hoteli nzuri,” alisema Kikwete.

Alisema baada ya mjadala wa kina walipata wazo la kufanyia mkutano huo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, ambapo walibuni mbinu za kuupamba na kuonekana ni ukumbi wa maana wa mikutano, tofauti na ulivyokuwa unaonekana kwa siku za kawaida.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi