loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mazito yaibuka ajali ya lori la mafuta

MAJERUHI 13 walionusurika katika ajali ya lori lililolipuka na kuua watu 76 hadi sasa hawajitambui, hatua ambayo imefanya ofi si ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kuingilia kati ili kumaliza utata ulioibuka kutoka kwa baadhi ya ndugu wa majeruhi hao.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 10, mwaka huu saa mbili na dakika 20 asubuhi baada ya lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 717 DDF, likiwa na trela namba T 645 CAN, likiwa limebeba mafuta ya petroli na dizeli kupinduka.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha alisema kuna baadhi ya watu wamejitokeza, ambao si ndugu wa marehemu wala majeruhi na kuzua utata.

“Tumealika watu waje kutambua miili au majeruhi ambao hawajitambui, cha kushangaza kuna watu ambao hawana uhusiano na ndugu lakini wamekuja sasa unakuta mtu mmoja wanajitokeza watu watatu mpaka watano na hawajuani,” alisema.

Aligaesha alisema kuwa kufuatia hali hiyo, wameomba msaada kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili waweze kuchukua vinasaba kwa ndugu waliojitokeza pamoja na majeruhi, ambao hawajitambui, pamoja na maiti.

“Mpaka sasa wagonjwa wote 13 ambao hawajitambui wameshachukuliwa vinasaba vyao, na ndugu zaidi ya 45 wameshachukuliwa vinasaba ambao tutalinganisha na miili ambayo ipo mochwari na wale ambao hawajitambui,” alisema.

Meneja wa Maabara ya Vinasaba (DNA) kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Hadija Mwema alisema sampuli linganishi zimechukuliwa kutoka kwa wazazi baba, mama na kuna baadhi ambao wazazi wao walishatangulia mbele za haki, hivyo wanachukua vinasaba kwa watoto na ndugu wa karibu kama baba mdogo, baba mkubwa, kaka ama dada.

“Kuna baadhi ya wenzetu wazazi wameshatangulia mbele za haki na kuna wengine bado hawajawa na watoto, teknolojia ya vinasaba inawezesha utambuzi kwa wale ndugu wa karibu kabisa, ndio zoezi linaloendelea hapa sasa,”alisema.

Alisema sampuli ya vinasaba imeshachukuliwa kwa miili yote, na pia ambao hawajitambui pia sampuli zimechukuliwa, kwa lengo la kulinganisha. Wakati huo huo, Eligaesha alisema majeruhi mwingine amefariki dunia usiku wa kuamikia jana na hivyo kufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 76.

Alisema majeruhi 13 walionusurika hali zao ni mbaya na wamelazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) wakiwa hawajitambui, huku 25 wakiwa wanaendelea vizuri. Alisema waliofariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili hadi sasa ni wanane.

“Hadi leo Agosti 13, hiyo ndiyo idadi ya wagonjwa waliolazwa MNH, na wale ambao wamefariki dunia tayari miili yao imepelekwa Morogoro na mmoja umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hapa Muhimbili,” alisema Aligaesha.

Wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo baada ya ajali walikuwa 45, wanaume wakiwa 41 na wanawake wanne. Tume ya uchunguzi yaanza kazi Katika tukio lingine; Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema tayari Waziri Mkuu amekamilisha kazi yake ya kuunda tume ndogo ya wataalamu, ambayo imeanza kazi zake na amewahakikishia Watanzania kuwa baada ya kukamilisha shughuli zake taarifa rasmi itatolewa kwa wananchi.

Waziri Jenista alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya jengo la kuhifadhia maiti la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo pia timu ya Kitaifa ya Maafa ilikabidhi rasmi timu ya maafa ya Mkoa wa Morogoro kuendelea kufanya kazi na hiyo wakati ya kitaifa ikiendelea kusimamia na kufuatilia wa maafa hayo.

Jenista alilazimika kutoa ufafanuzi wa shughuli za tume ndogo ya wataalamu, iliyoundwa na Majaliwa ambayo aliipa siku sita kuchunguza namna ya uwajibikaji wa viongozi uliochukuliwa kabla ya ajali ya lori mafuta na kusababisha vifo vya watu wengi na kujeruhi wengine. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo Agosti 11 mwaka huu, alipotoa salamu za pole kwa niaba ya Rais John Magufuli.

Alisema ripoti ya tume hiyo, itaisaidia serikali kuchukua hatua ya viongozi na watendaji walishindwa kuwajibika kikamilifu kutokana na ajali hiyo. Jenista alisema: “Tutatoa taarifa rasmi kwa sababu tayari Waziri Mkuu amekamilisha na amekabidhi jukumu kwa tume na tutaweka utaratibu wa kuripoti kazi za tume”.

MFANYABIASHARA Tariq Machibya (29) ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi