loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tani 20 za pamba zakamatwa zikitoroshwa

GARI lenye zaidi ya tani 20 za pamba zilizonunuliwa kwa magendo na baadaye kusafi rishwa bila kufuata utaratibu limekamatwa jana saa nne usiku katika Kata ya Dutwa wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Gari hilo lenye namba za usajili T 917 BCN lilipakia pamba hiyo iliyokuwa imekusanywa nyumbani kwa mtu katika kata ya Gilya wilayani Bariadi kinyume na utaratibu uliowekwa na Bodi ya Pamba ambapo utaratibu umeelezwa kuwa pamba yote inatakiwa kununuliwa kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS).

Akizungumza katika eneo la tukio jana, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisema kuwa gari hilo lilikamatwa likiwa linasafirisha pamba hiyo kinyume na utaratibu. Kiswaga alisema kuwa kutokana na hali hiyo aliliagiza Jeshi la Polisi kulishikilia gari hilo pamoja na dereva mpaka pale wamiliki na wanunuzi wa pamba hiyo watakapopatikana.

“Naliagiza Jeshi la Polisi kuendelea kulishikiria gari hilo pamoja na dereva huku wakiwasaka wanunuzi wa pamba hiyo watafutwe ili waje kujibu kosa hilo la kununua na kusafirisha kimagendo pia nawasihi wanunuzi hao wajitokeze mara moja na kujisalimisha wenyewe,” aliagiza Kiswaga.

Aidha, dereva wa gari hilo, Lulyalya Deus alieleza kutowafahamu wanunuzi wa pamba hiyo kwa kusema alilipwa malipo ya kazi ya kusafirisha na kukiri kushuhudia pamba hiyo ikipakiwa kwenye gari na kwamba watu hao walitoroka pindi gari hilo liliposimamishwa kwa ajili ya ukaguzi.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi