loader
Picha

SHONZA AITA WAWEKEZAJI SOKA LA WANAWAKE

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema ubingwa wa Cosafa iliyotwaa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘Tanzanite’ ni funzo kuwa uwekezaji unahitajika zaidi kwao.

Tanzanite iliyoshiriki michuano hiyo ya Baraza la Soka kwa nchi za Kusini mwa Afrika kama timu mwalikwa, ilitwaa ubingwa huo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuichapa Zambia mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa Afrika Kusini.

Akizungumza juzi baada ya kuipokea timu hiyo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Shonza alisema walichokifanya wachezaji hao ni fursa na funzo kwamba kumbe wakiwekeza timu ya wanawake wanaweza kutangaza nchi kimataifa.

“Vijana wetu wamefanya kazi kubwa sana, sisi kama Wizara tunawapongeza kwasababu walishiriki kama wageni waalikwa lakini hawakubweteka kuona hayawahusu, wamepambana na kutwaa ubingwa,”alisema.

TIMU ya Tanzania Bara ya wasichana walio chini ya Umri ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi