loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yaanza mikakati kuwang’oa Rollers

KIKOSI cha Yanga kimeenda kukita kambi mkoani Kilimanjaro kujiandaa na mchezo wa marudiano wa ugenini kwa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Agosti 24 mjini Gabarone, Botswana ikiwa ni baada ya Yanga kupata sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza nyumbani mwishoni mwa wiki.

Kikiwa mkoani humo, kinatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania na dhidi ya AFC Leopard ya Kenya kujiweka fiti kabla ya kusafiri kwenda kuwakabili wapinzani wao Rollers.

Katika mchezo huo, Yanga wameapa kufia uwanjani kupata matokeo chanya yatakayowafanya kutinga hatua inayofuata huku kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera akiwaahidi mashabiki kwenda kuvuna ushindi kwenye mchezo huo wa ugenini.

Yanga wameamua kuweka kambi Kilimanjaro ili kuzoea hali ya hewa ya baridi iliyopo Botswana.

Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alithibitisha kuondoka kwa kikosi hicho kwenda Kilimanjaro kikiwa na nyota wao wote akiwemo Juma Abdul na Kelvin Yondani waliositisha mgomo wao wa kudai fedha zao na kuungana na wenzao.

“Katika kuhakikisha kikosi chetu kinajiandaa kwa mchezo wa marudiana tumeona iende kuweka kambi Kilimanjaro na kimeondoka leo asubui (jana) na kikosi chote kipo fiti na wachezaji Juma Abdul na Kelvin Yondani watakuwa sehemu ya kikosi na tunaendelea kumalizana na Vincent Dante kuhakikisha anakuwa sehemu ya kikosi,” alisema Mwakalebela. Alisema michezo hiyo miwili ya kirafiki inatarajiwa kuanza kuchezwa mwishoni mwa wiki hii.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi