loader
Picha

Mabalozi 42 kutembelea mradi umeme Rufiji leo

MABALOZI 42 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali leo watatembelea mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufi ji uitwao Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kuona utekelezaji wa mradi huo na kasi ya mapinduzi ya uchumi wa viwanda.

Aidha, ziara hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kutumia diplomasia ya uchumi kupitia mabalozi hao katika nchi waliko, kuhakikisha wanaleta wawekezaji wengi nchini kutokana na uhakika wa umeme utakaotokana na mradi huo.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbas aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa mabalozi hao tayari wapo nchini na leo watakwenda Rufiji kuona mradi huo. “Mabalozi wanaiwakilisha nchi yetu duniani. Tanzania hivi sasa inakwenda kasi katika mapinduzi ya viwanda. Wakirudi katika nchi wanakoiwakilisha nchi watakuwa na kazi ya kuleta wawekezaji zaidi kama tunavyojua wao ni mabalozi na wanatekeleza diplomasia ya uchumi,” alisema Dk Abbas.

Mradi wa JNHPP unaogharimu Sh trilioni 6 ni wa kimkakati, unaosadia kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa ajenda ya viwanda katika SADC, ikiwa ni sehemu ya Mkakati wa Viwanda wa wa mwaka 2015-2063, unaotekelezwa kwa awamu mbili (2015-2030 na 2030-2063). Mradi huo wa Rufiji utazalisha megawati 2,115.

Katika hatua nyingine, Dk Abbas alisema nchi zote 16 zinazounda SADC, zimethibitisha kushiriki katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 17na 18. “Napenda kuchukua fursa hii kuwatangazia ramsi kuwa akidi imetimia, marais, wakuu wa serikali na wafalme wa SADC wote wamethibitisha kushiriki mkutano huo,” alisema Dk Abbas.

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi