loader
Picha

RC Pwani kuanza ukaguzi viwanda 14 leo

MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo anaanza ziara ya siku tisa ambapo anakutembelea viwanda 14 vilivyojengwa mkoani humo kuanzia leo Jumatano, Agosti 14, 2019 hadi Agosti 22, 2019.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Theresia Mbando ziara hiyo inahusisha viwanda 14 kati ya 1,192 vilivyopo mkoani Pwani.

Mbando amesema kati ya viwanda hivyo, vikubwa ni 56, vya kati 85, vidogo ni 350 na vidogo zaidi ni 701 vikiwa vimejengwa kwenye wilaya zote mkoani humo.

RAS amesema kuwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Magufuli la ujenzi wa viwanda ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

Amesema kuwa viwanda hivyo viko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi huku vingine vikiwa vimeanza uzalishaji ambavyo ni Lake Steel, Shafa Investment na Super Meals.

Aidha amesema kuwa katika ziara hiyo, mkuu huyo wa mkoa atatembelea viwanda 14 ambapo ataweka mawe ya msingi katika viwanda 13 na kimoja atakikagua ujenzi wake.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi