loader
Picha

Shein ataka maelezo wanafunzi kufeli mitihani

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kufanya utafi ti zaidi na kujua chanzo cha baadhi ya shule za Zanzibar wanafunzi wake kufanya vibaya na kushika nafasi za mwisho kitaifa katika mitihani yao.

Akilihutubia Baraza la Iddi Dole Kizimbani juzi, Rais Shein alisema hajaridhishwa matokeo mabaya ya baadhi ya shule za Zanzibar ambazo wanafunzi wake walishika nafasi za mwisho.

Alisema haoni sababu kwa nini wanafunzi washike nafasi za mwisho huku elimu ikitolewa bure huku vifaa vyote vya maabara kwa wanafunzi na michango ya ada ikiwa imefutwa.

“Nauagiza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kufanya utafiti kujua sababu za msingi za wanafunzi shule za Zanzibar kufanya vibaya mitihani ya kidato cha sita,” alisema.

Ili kujenga mazingira mazuri kwa wanafunzi wa shule za sekondari kufanya vizuri mitihani ya taifa, serikali imefuta michango ya ada yote ya shule waliyokuwa wakichangishwa wazazi.

Aidha mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara ya Elimu imetenga bajeti ya Sh bilioni 130 kwa ajili ya ada za wanafunzi kulipia vifaa ikiwemo madaftari na vitabu vya masomo ya sayansi.

Ofisa anayeshughulikia elimu ya wanafunzi wa sekondari ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema wamelipokea agizo hilo na wanatarajia kukaa kulijadili na kulifanyia kazi.

Akitangaza matokeo ya kidato cha sita ya mitihani iliyofanyika Mei, mwaka huu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alizitaja shule za Zanzibar zilizoshika nafasi za mwisho kitaifa kuwa ni Haille Sellasia,Tumekuja zilizopo eneo la Mji Mkongwe na Mwenge, Kimbe Samaki na Mpendae.

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi