loader
Picha

Wanawake watakiwa kunyonyesha watoto miaka 2

MKUU wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja, Rajab Ali Rajab amewaomba akinamama kuzingatia unyonyeshaji wa watoto ili kuwawezesha kukua vizuri wakiwa na afya njema.

Alisema hayo Bumbwini Kiongwe Mkoa wa Kaskazini B Wiki ya Unyonyeshaji ambayo lengo lake ni kuongeza hamasa wanawake kunyonyesha watoto kwa kutumia ziwa la mama.

Alisema wapo akinamama hawatumii fursa ya kuwanyonyesha watoto wao bila ya sababu za msingi na hiyo huchangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa afya ya mtoto na pia kuumwa.

Alizipongeza taasisi na asasi za kiraia kwa kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu unyonyeshaji wa mtoto na faida zake.

“Mtoto ndiyo taifa la kesho kwa hivyo akinamama mnatakiwa kuwanyonyesha kwani maziwa ya mama yamekamilika kwa kuwa na kila aina ya virutubisho,” alisema.

Akizungumza katika Wiki ya Unyonyeshaji, Ofisa Miradi wa taasisi ya Milele Foundation, Eshe Haji Ramadhan alisema wataelekeza juhudi zao kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na halmashauri za wilaya kuona huduma za afya na elimu inayafikia makundi yote.

“Tumejipanga vizuri kuona elimu kwa akinamama ikiwemo unyonyeshaji kwa kutumia ziwa la mama inawafikia walengwa ili kuona afya ya mtoto inakuwa bora,” alisema.

Ofisa wa lishe kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Said Salum Othman alisema takwimu zinaonesha kwamba hali ya unyonyeshaji kwa akina mama Zanzibar ipo kwa asilimia 30.

“Kiwango cha unyonyeshaji kwa akinamama kwa watoto kinapungua na kipo kwa asilimia 30 na wapo akinamama wengine hawafikishi miaka miwili ya kuwanyonyesha watoto,”alisema

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi