loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchakato ujenzi wa hospitali iliyopewa fedha na JPM waanza

MCHAKATO wa matumizi ya Sh bilioni 1.5 zilizotolewa wa Rais John Magufuli (JPM) kwa ajili ya ujenzi wa hospitali itakayozishirikisha kata za Buseresere na Katoro mkoani Geita na kuwanufaisha wakazi zaidi ya 100,000 umeanza.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Said Kalidushi, alisema hayo juzi jioni wakati wa mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Chato, Dk Medadi Kalemani, uliofanyika katika Kata ya Buseresere wilaya ya Chato mkoani Geita na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wakiwemo viongozi wa chama na serkali wa kata za Katoro na Buseresere.

Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo Kalidushi alisema zilitolewa na Rais Magufuli mwezi uliopita alipokuwa mkoani Geita kufuatia kilio cha wakazi wa kata hizo zenye wakazi 100,000 ambao wamekuwa hawana hospitali yenye hadhi ya wilaya pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu.

“Hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi..hatua hii ndiyo inayowafanya viongizi wa CCM kutembea vifua mbele kwani hiyo inatosha kuthibitisha kuwa ahadi zinatekelezeka mbali na mkakati wa ujenzi wa zahanati kwa kila kata kote nchini,” aliisema Kalidushi.

Kwa upande wake, Dk Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati akielezea serikali inavyotekeleza Ilani ya C CM chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli alisema kumekuwepo na mabadiliko makubwa kuanzia ngazi za vijiji, kata na hata wilaya ikiwemo kuboreshwa kwa huduma za kijamii.

Aliwaomba Watanzania waendelee kumuamini Rais Magufuli kwani wao ni mashuhuda katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wake kumekuwa na mafanikio makubwa kama kurejea kwa nidhamu kwa watumishi wa umma, kujali maslahi yao na kuboreshwa kwa huduma za kijamii ambapo kila kunapokucha mambo makubwa yanafanyika.

Awali wakati wa ufungunzi wa mkutano huo, Diwani wa Kata ya Buseresere, Godfrey Miti, aliyekuwa pia mwenyeji wa mkutano huo aliwahakikishia wananchi kuwa baadhi ya ahadi zilizotekelezwa ni pamoja na kwenye kata yake yenye vijiji saba, ambapo tayari kila kijiji kina visima viwili wakati juhudi za utekelezaji mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria zikifanyika, Aliyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutekelezwa kwa mpango mkakati wa kila kijiji kuwa na zahanati unaoendelea sanjari na kukamilika kwa ujenzi sekondari ya pili katika kata hiyo ya Mulanda ambayo tayari imeshahaanza kupokea wanafunzi na wameanza masomo.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa ujenzi wa hospitali kwa kata za Katoro na Buseresere kwa fedha zilizotolewa na Rais Magufuli alisema mipango ipo katika hatua ya mwishio ya kutenga eneo itakapojengwa.

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vyombo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Chato

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi