loader
Picha

SBL yaanza kupanda miti 1,000

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni maalumu ya kupanda miti 1,000 mkoani Kilimanjaro, ili kulinda vyanzo vya maji na uoto wa asili mkoani hapa.

Kampeni hiyo itakayotekelezwa kwa ushirikiano na taasisi ya The Kilimanjaro Project imelenga kuihamasisha jamii kuongeza jitihada za kutunza mazingira.

Akizindua kampeni hiyo katika Kiwanda cha SBL mjini Moshi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mark Ocitti, alisema wanatarajia kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira katika maeneo mengine nchini.

“SBL imejizatiti kurejesha uoto wa asili kwa kushirikiana na wadau wengine kuhifadhi vyanzo vya maji na baadaye tutakwenda wilaya ya Mwanga kuendeleza kampeni,” alisema.

Alisema mpango huo wa SBL unakwenda sanjari na sera yake ya kurudisha kwa jamii sehemu ya faida, na umejikita zaidi katika utoaji wa huduma bora ya maji safi kupitia mradi uitwao Water of Life (WOL).

Mradi wa WOL umelenga kuwasaidia wanafunzi kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, kuwasaidia wakulima wa ndani hususani wa vijijini pamoja na mpango wa kuhamasisha unywaji pombe kistaarabu.

Aidha upandaji miti umehudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sara Cooke pamoja na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza Kitengo cha Biashara, Andrew Rosindell, ambao walikuwa ziarani kiwandani hapo.

Mkurugenzi huyo alisema upandaji miti linakuja huku kukiwa na wito kutoka jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kuongeza juhudi za uhifadhi wa misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi