loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaodaiwa kodi ya ardhi walipe haraka

WAMILIKI wa Mbeya Hoteli ya jijini Mbeya, wameahidi kulipa ziada ya kodi wanayodaiwa kama kodi ya pango la ardhi wanayomiliki.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwataka wadaiwa sugu wote wa kodi ya pango la ardhi nchini kulipa.

Wamiliki hao wamesema wako tayari kulipa kiasi kinachodaiwa, kwa kuwa awali waliamini Sh 63,000 walizokuwa wakilipa, ndio sahihi hadi ilipobainika wanatakiwa kulipa Sh milioni 6.3.

Tumeguswa na hatua ya wamiliki hao, kukiri kosa na kuamua kulipa kiasi kilichopungua kwa kodi ambayo wamekuwa wakilipa huko nyuma. Tunaungana na wadau wa masuala ya ardhi na kodi, pia kuwapongeza na kutaka wadaiwa zaidi wa miamala ya ardhi, kulipa kodi wanayodaiwa.

Ni vizuri watu na taasisi za umma na binafsi, zinazomiliki ardhi nchini wakaelewa umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi kwa maendeleo ya nchi.

Na wakishajua hivyo, ni vizuri kila mmoja bila kulazimishwa, wakajenga utamaduni wa kulipa kodi yote wanayodaiwa na kwa wakati muafaka.

Haipendezi Waziri Lukuvi kukaa anatumia muda mwingi, kuwasaka wadaiwa wote sugu wa pango la ardhi, ilihali kila mmoja anajua wajibu.

Tumsaidie Waziri Lukuvi kuendeleza sekta ya ardhi, kwa kupima viwanja katika maeneo mengi zaidi nchini, kwa kumwezesha kwa kulipa kodi.

Kufanya kinyume chake ni kuhujumu jitihada zake nzuri, anazozichukua kusafisha uozo, ambao umeigubika sekta ya ardhi miaka nenda rudi.

Ni muhimu wamiliki wa ardhi nchini, wakajua umuhimu wa vipande walivyomilikishwa kwa maisha yao na kuvitendea haki kwa kuvilipia.

Kama ambavyo hakuna anayekumbushwa kula, basi iwe ni kama ada pia kwa watu kulipa kodi ya ardhi, kwani maisha yao yanategemea ardhi.

Ni matarajio yetu kuwa hatua ya wamiliki wa Mbeya Hoteli kulipa kodi yao itafungua ukurasa wa wadaiwa zaidi sugu kulipa madeni yao yote.

Na si kulipa madeni tu, bali wale wenye ardhi ambayo vipimo vyake haviko sahihi na hivyo hulipa kiasi kidogo cha kodi ya ardhi waseme.

Kujitokeza kwao kusema ukweli, kutathibitisha nia yao safi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kukusanya mapato mengi.

Ni matarajio yetu baada ya Waziri Lukuvi kutoa orodha ya watumishi wa wizara yake, ambao wamekuwa wakiingilia mfumo wa malipo, watakaoendelea kuficha ukweli wa madeni yao, tutawahesabu wanadhamiria kuhujumu uchumi.

Chonde chonde wamiliki wote wa ardhi nchini, angalieni miamala yenu na kurekebisha kasoro zinazofanya baadhi yenu mlipe kodi ndogo na hivyo kuinyima serikali mapato inayostahili.

Hatupendi kuamini katika awamu hii makini ya Rais Dk John Magufuli, bado kuna watu ambao wanatamani kuendelea kuidanganya serikali.

KUANZIA leo hadi Jumapili wiki hii jijini Dodoma, Chama Cha ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi