loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkapa kueleza uzoefu wake SADC

MWENYEKITI mstaafu wa SADC na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, kesho atatoa mhadhara kwa umma kuhusu uzoefu wake katika jumuiya hiyo.

Mhadhara huo utakaowashirikisha wasomi, wachambuzi wa masuala ya kikanda, wanasiasa, wachumi, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida, utafanyika katika jengo jipya la maktaba la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Taarifa iliyotolewa mwanzoni mwa wiki kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) ilieleza kuwa mhadhara utawashirikisha jopo la watu wenye uzoefu wa masuala ya SADC, akiwemo Katibu Mtendaji mstaafu wa SADC, Dk Simba Makoni.

Wengine ni Profesa Anthoni van Nieuwkerk, Mratibu wa Masomo ya Usalama katika Shule ya Utawala ya Wits (Wits School of Governance), Afrika Kusini na Gilead Teri mtaalamu wa Kuendeleza Sekta Binafsi Tanzania kutoka Benki ya Dunia.

Mhadhara huo ulioandaliwa na SADC, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) na UDSM, umelenga kuchochea na kuhamasisha mjadala kuhusu mtangamano wa kikanda hasa unaohusu SADC.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Uongozi, majadiliano yatajikita katika mafanikio endelevu ya mtangamano, fursa, changamoto zilizo vikwazo kwa mtangamano na namna ya kukabiliana nazo.

“Uzoefu kutoka kwa jumuiya nyingine ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa malengo ya SADC,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, ratiba ya Sekretarieti ya SADC inaonesha kuwa, Agosti 16 kutafanyika mkutano wa marais wa utatu wa TROIKA unaohusika na masuala ya siasa (demokrasia) ulinzi na usalama.

MFUMO wa kielektroniki wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi